work from home opportunities, mom work at home, home from work, looking for work from home, get paid, i want to work from home, work at home ideas, work from home programs, work at home jobs, work from home online, work from home opportunities, online work
Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma imeendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa Vyuo mbalimbali nchini kuhusu utaratibu wa mchakato wa ajira Serikalini kwa lengo la kuwajengezea uelewa na uwezo wa masuala yanayohusu mchakato wa ajira katika utumishi wa umma.
Chanzo: Public service Recruitment Secretariat
Matangazo Mapya ya Ajira Bofya hapa
Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma imeendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa Vyuo mbalimbali nchini kuhusu utaratibu wa mchakato wa ajira Serikalini kwa lengo la kuwajengezea uelewa na uwezo wa masuala yanayohusu mchakato wa ajira katika utumishi wa umma.
Akizungumza katika mahafali ya
Jumuiya ya wanafunzi wa Taasisi za Vyuo vikuu Tanzania (TAHILISO)
yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Katibu msaidizi wa Sekretarieti hiyo
Bibi Khadija Isihaka ameeleza kuwa, wahitimu wa vyuo vikuu ni moja ya
wadau wakubwa wa Sekretarieti ya ajira ambao wanapaswa kujua utaratibu
wa ajira Serikalini na namna ya kutuma maombi ya kazi pindi nafasi wazi
zinapotangazwa.
“Katika Utekelezaji wa majukumu
ya Sekretarieti ya ajira, wahitimu wa Vyuo vikuu ni wadau muhimu kwetu,
hivyo ni wajibu wetu kuwapa uelewa kuhusu utaratibu wa ajira katika
Utumishi wa Umma” alisema Isihaka.
Katika mahafali hayo wahitimu
hao walipata fursa ya kujua mambo mbalimbali yanayohusu utaratibu
unaotumika kutuma maombi ya kazi kwa njia ya kielektroniki ‘Recruitment
portal’, uandaaji wa wasifu binafsi (CV), umuhimu wa kuambatanisha
nyaraka muhimu kama vyeti vya kitaaluma wakati wa kutuma maombi yao ya
kazi na mambo muhimu wanayopaswa kuzingatia wakati na kabla ya usaili.
Katika halfa hiyo, wahitimu
kutoka vyuo mbalimbali walipata fursa ya kujua majukumu ya Sekretarieti
ya Ajira na umuhimu wa kufungua akaunti kwenye mfumo portal ya ajira
unaopatikana kwa anuani ya https://portal.ajira.go.tz kwa ajili ya kuingiza taarifa zao zitakazowasaidia kuwasilisha maombi ya kazi katika mfumo huo pindi zinapotangazwa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa umma, 22 Mei, 2017Chanzo: Public service Recruitment Secretariat
Matangazo Mapya ya Ajira Bofya hapa