Details 
Business / Employer name: Expert Consultancy on Behalf of the Client
Job categories: Manufacturing
Description
Kwa niaba ya mteja wetu mwenye kiwanda cha uzalishaji wa vyuma katika wilaya mkuranga tunahitaji mafundi umeme wa kufanya kazi za umeme kiwandani.
Majukumu ya Muombaji:
 Kufanya ufungaji, matengenezo na marekebisho ya vifaa vitumiavyo umeme kwa kuzingatia viwango vya usalama ipasavyo.
 Kutunza vitendea kazi, kupima vifaa vya umeme na kuhakikisha vipo salama muda wote;
 Kufunguwa na kutunza kadi za vitendea kazi vya umeme;
 Kufunga, kurekebisha na kusimamia mfumo wa uwekwaji umeme na vifaa vyake
 Kuchunguza na kutafuta makosa yanayopelekea mfumo wa umeme kutokufanya kazi
 Kuhakikisha udhaifu katika mfumo hautokei kwa kufanyia kazi makosa madogo madogo
 Kutengeneza michoro ya uwekaji nyaya, michoro ya itakavyokuwa na miongozo maususi ya kiufundi kwa ajili ya mfumo au marekebisho ya vifaa na mpangilio maalumu wa mtu anayeshughulikia uwekajia na marekebisho ya umeme.
 Kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa mfumo wa umeme, vifaa vya umeme na kutoa mapendekezo au kuweka utaratibu wa marekebisho au kubadilisha kifaa chenye tatizo.
Sifa za muombaji
 Awe na stashahada/cheti/vigezo vya VETA katika fani ya umeme
 Umri usiozidi miaka 45 tangu kuzaliwa.
 Ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.

 KUTUMA MAOMBI BOFYA HAPA 
 
 
Top