Join Facebook More Jobs
post a job, job postings,job search, job vacancies, job search sites, job search websites,local job search, post a job, job postings,job search, job vacancies, job
More Jobs Vacancies
post a job, job postings,job search, job vacancies, job search sites, job search websites,local job search, post a job, job postings,job search, job vacancies, job
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa
yeyote anayetaka kuwa Mdadisi au Mkusanyaji taarifa za kitakwimu rasmi
katika tafiti mbalimbali zinazoratibiwa na ofisi hii, ni sharti awe
amehitimu Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi angalau kwa ngazi ya
cheti.
Hii
ni kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya kuratibu na kusimamia ukusanyaji takwimu
rasmi (official statistics) nchini.
Hivyo,
kuanzia sasa NBS itakuwa inawatumia wadadisi ambao wamehudhuria na
kuhitimu angalau cheti cha Ukusanyaji Takwimu katika miradi mbalimbali
ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
Mafunzo
ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki
mwa Afrika “Eastern Africa Statistical Training Centre” (EASTC)
kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano zaidi na kujisajili wasiliana na:
Ofisi ya Msajili wa Chuo,
Eastern Africa Statistical Training Centre,
S.L.P 35103,
DAR ES SALAAM.
Barua pepe: info@eastc.ac.tz;
Tovuti: www.eastc.ac.tz
Simu namba: 022-2925000 au 0784784106.
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
DAR ES SALAAM.
More Jobs Vacancies