post a job, job postings,job search, job vacancies, job search sites, job search websites,local job search, post a job, job postings,job search, job vacancies, job
Description
TEMISE Tanzania na HERTU Investment ni taasisi zinayojihusisha na kilimo biashara endelevu. Zimejikita katika kuzalisha Uyoga, Matunda, Mbogamboga na ufugaji wa Kuku wa kienyeji na bidhaa zake kibiashara. Pia hutoa huduma ya mafunzo, ushauri wa kukuza na kuendeleza biashara; kubuni, kuanzisha, kusimamia miradi mbalimbali, pamoja na kuandaa mipango/michanganuo ya biashara, na maandiko ya miradi.
Dar es Salaam
a) Kusaidia kuandaa mikakati na malengo ya mauzo/masoko
b) Kubuni mbinu mbalimbali za kuuza bidhaa na kufikia wateja wengi
c) Kutafuta masoko, kuuza na kusambaza bidhaa za taasisi
d) Kutangaza bidhaa na kutafuta wateja
e) Kuandaa ripoti mbalimbali za mauzo na masoko
f) Utunzaji kumbukumbu wa bidhaa, wateja na mauzo
g) Kutekeleza kazi zingine atakazopangiwa na taasisi
a) Awe na elimu ya ngazi ya kidato cha nne na kuendelea. Akiwa na cheti au stashahada mchepuo wa masoko na mauzo itakuwa sifa ya ziada kwa mwombaji.
b) Awe na ari na bidii ya kupata kipato kikubwa kwa kufanya mauzo mengi
c) Uelewa mzuri na ueledi wa kuimarisha na kupanua wigo wa masoko
d) Awe na uzoefu wa zaidi ya mwaka mmoja na zaidi katika mauzo na masoko ya bidhaa mbalimbali
e) Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
f) Awe na sifa kujituma,mwaminifu, mbunifu na uwezo mkubwa wa kujieleza, ushawishi na kujenga mahusiano.