Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) imetangaza nafasi za kazi 10,000 kwa wananchi wote waliopo nchini kwenye mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutokea Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga.
Hayo yamebainisha na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TaESA, Boniface Chandaruba wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuwataka watanzania kujitokeza kujisajili ambapo zoezi hilo limeshaanza kuanzia sasa na litasitishwa  Machi 30, 2018  ili waweze kuwatambua rasmi.
Aidha, Mradi huo unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 24 hadi 36 na unategemewa kuzalisha fursa za ajira takribani 10,000 wakati wa ujenzi na ajira zaidi ya 1,000 wakati wa uendeshaji wake.
Pamoja na hayo, Chandaruba ameendelea kwa kusema "nafasi hizi ni nafasi ambazo haziitaji gharama yeyote ile katika kujisajili au kutambuliwa".
Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi  “East Africa Crude Oil Pipeline (EACOP)”  kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga nchini Tanzania unategemewa kuwa na urefu wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba hilo utafanyika nchini Tanzania. Jumla ya wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.
Jinsi ya Kutuma Maombi Bofya Hapa
 TaESA job, Job in Morogoro, TaESA job,Job in Morogoro, TaESA job, TaESA job, TaESA job,TaESA job,Government job, Government job,
 
 
Top