Location
Arusha Mjini Arusha
Description
Arusha Beverages Co. Ltd ni kampuni inayozalisha na kusambaza kinywaji aina ya ‘FARU’ kinachotokana na zao la ndizi. Arusha Beverages Co. Ltd inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi ya Dereva Mauzo kwa wale wote wenye vigezo vifuatavyo;
SIFA ZA MUOMBAJI:
  1. Muombaji anatakiwa awe na cheti cha taaluma husika yaani mauzo kwa kiwango cha certificate.
  2. Cheti cha kidato cha nne au sita.
  3. Leseni ya udereva daraja “D” ingawa “C” inapendekezwa zaidi.
  4. Uzoefu wa kuendesha magari ya mizigo (mfano: Suzuki carry, Fuso, Canter, Scania n.k) kwa muda usiopungua miaka miwili bila kusabisha ajali (suala hili litafuatiliwa katika kitengo cha usalama barabarani ikiwa ajira itapatikana).
  5. Awe mwenyeji wa mkoa wa Arusha. (Hii ni lazima)
  6. Awe na uzoefu wa kuuza vinywaji vitokanavyo na zao la ndizi yaani Banana kutoka katika kiwanda chochote. (Hii ni lazima)
  7. Pia awe na uelewa mzuri wa alama za barabarani.
  8. Awe mchapa kazi, mwadilifu na mwenye kuzingatia muda.
 Apply  Now 
driving job, driver job, home from work, Driving job, get paid, drive job
 
Top